Munich, Ujerumani
Robert Lewandowski ameshindwa kuibeba Barcelona katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya timu hiyo kulala kwa mabao 2-0 dhidi ya Bayern Munich mechi iliyopigwa usiku wa Jumanne kwenye dimba la Allianz Arena.
Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Lewandowski kurudi Allianz Arena tangu aachane na Bayern Julai mwaka huu na kutua Barcelona ambapo kabla ya mechi hiyo mashabiki wengi walikuwa wakijiuliza nini atafanya mchezaji huyo aliyeshinda karibu kila kitu katika miaka yake minane na klabu hiyo ya Munich.
Katika mechi hiyo Lewandowski alipoteza nafasi kadhaa huku Barcelona ikionekana kuzidiwa na wapinzani wao hasa kipindi cha kwanza kabla ya kuadhibiwa na mabao ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Lucas Hernandez na Leroy Sane.
Katika mechi nyingine, Liverpool imetema cheche baada ya kuichapa Ajax mabao 2-1 ikineemeka na mabao ya Mohamed Salah katika dakika ya 17 lakini Ajax waliokuwa ugenini walisawazisha kupitia kwa Kudus dakika 10 baadaye lakini alikuwa Joel Matip aliyeihakikishia Liverpool bao la ushindi katika dakika ya 89.
Matokeo ya mechi za Jumanne za Ligi ya Mabingwa ni kama ifuatavyo…
Sporting 2-0 Tottenham
Liverpool 2-1 Ajax
Bayern Munich 2-0 Barcelona
Viktoria Plzen 0-2 Inter Milan
B Leverkusen 2-0 Atl Madrid
FC Porto 0-4 Club Bruge
Kimataifa Bayern pagumu kwa Lewandowski
Bayern pagumu kwa Lewandowski
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
