London, England
Kocha Thomas Tuchel amesema kwamba kitendo cha klabu ya Chelsea kumfuta kazi baada ya matokeo mabaya ya msimu huu kimemvuruga.
Tuchel alifutwa kazi Jumatano iliyopita baada ya timu yake kufungwa bao 1-0 na Dinamo Zagreb katika mechi ya Lagi ya Mabingwa Ulaya na siku iliyofuata mabosi wa Chelsea wakampa nafasi hiyo kocha wa Brighton, Graham Potter.
“Hii ni kati ya taarifa ngumu ambayo nimewahi kuiandika na ni taarifa ambayo natumaini sitohitaji kuiandika kwa miaka mingi, nimevurugwa baada ya kuona muda wangu katika klabu ya Chelsea umefikia mwisho,” alisema kupitia mtandao wa Twitter na kuongeza, “Hii ni klabu ambayo nilijiona niko nyumbani, kikazi na kwangu binafsi.”
Tuchel alijiunga na Chelsea Januari mwaka jana akichukua nafasi ya Frank Lampard, matunda yake yalianza kuonekana mapema na hatimaye akaifikisha timu hiyo katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufanikiwa kuilaza Manchester City.
“Ninachojivunia na kukifurahia kwa sasa ni kuisaidia timu kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, na taji la Klabu la Dunia, hayo yataendelea kuwa katika fikra zangu siku zote,” alisema.
“Nimepata heshima ya kuwa sehemu ya historia ya klabu hii na kumbukumbu za miezi 19 iliyopita itaendelea siku zote kuwa kitu maalum katika moyo wangu,” alisema.
Kimataifa Tuchel akiri Chelsea wamemvurga
Tuchel akiri Chelsea wamemvurga
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
