London, England
Ikiwa nyumbani Old Trafford Alhamisi hii Man Utd imeanza vibaya mbio za kusaka heshima katika Europa Ligi baada ya kulala kwa bao 1-0 mbele ya Real Sociedad wakati Arsenal ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya FC Zurich
Mechi ya Man Utd ambayo awali kulikuwa na fununu kwamba isingechezwa kutokana na kifo cha Malkia Elizabeth 11 lakini mazungumzo baina ya FA na Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) hatimaye yaliwezesha kuchezwa kwa mechi hiyo ambayo ilikuwa mbaya kwa Man Utd.
Mechi hiyo ilichezwa bila ya kuwapo shamrashamra za muziki na wachezaji walivaa vitambaa vyeusi na kutoa heshima ya dakika moja kwa ajili ya kumkumbuka Malkia Elizabeth 11 ambaye amefariki Alhamisi akiwa na miaka 96.
Alikuwa ni Brais Mendez aliyeibeba Sociedad katika dakika ya 59 kwa bao la mkwaju wa penalti ambayo ilitolewa baada ya Lisandro Martinez kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Wakati mambo yakiwa mabaya kwa Man Utd, Arsenal wao wakiwa ugenini walizianza vizuri mbio za Europa Ligi baada ya kuichapa FC Zurich mabao 2-1.
Arsenal ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 16 ya mchezo lililofungwa na Oliveira Alencar akiutumia vizuri mpira ulioanzia kwa Eddie Nketiah lakini Zurich walisawazisha kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Mirlind Kryeziu dakika moja kabla ya mapumziko, penalti hiyo ilitolewa baada ya Nketiah kumchezea rafu Ola Selnaes.
Hata hivyo alikuwa ni Nketiah aliyerudisha matumaini Arsenal katika dakika ya 62 baada ya kuipatia timu hiyo bao la ushindi akiujaza mpira wavuni kwa kichwa kufuatia krosi ya Marquinho.
Matokeo ya mechi za Europa Ligi za Alhamisi hii ni kama ifuatavyo
Zürich 1-2 Arsenal
Man Utd 0-1 Real Sociedad
PSV Eindhoven 1-1 Bodø/Glimt
AEK Larnaca 1-2 Rennes
Fenerbahce 2-1 Dynamo Kyiv
HJK Helsinki 0-2 Real Betis
Ludogorets 2-1 Roma
Union Berlin 0-1 Union Saint-Gilloise
Malmö FF 0-2 Sporting Braga
Omonia Nicosia 0-3 Sheriff Tiraspol
Lazio 4-2 Feyenoord
Sturm Graz 1-0 Midtjylland
Kimataifa Europa ngumu Man Utd, tamu Arsenal
Europa ngumu Man Utd, tamu Arsenal
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
