Na mwandishi wetu
Kuelekea pambano lake la Septemba 24, mwaka huu dhidi ya Abdo Khaled, bondia Twaha Kassim ‘Kiduku’ amewahakikishia ushindi Watanzania akiwaahidi kutowaangusha akijinasibu kuwa yupo tayari kwa pambano.
Pambano hilo la ubingwa wa UBO Afrika la uzito wa kati linatarajia kufanyika kwenye dimba la Nangwanda Sijaona, Mtwara likiwa la raundi 10.
Akizungumza na GreenSports, bondia huyo mwenyeji wa Morogoro alieleza kwamba yupo kwenye mazoezi makali na amejiandaa vya kutosha kuhakikisha anaiwakilisha vyema Tanzania dhidi ya mpinzani wake huyo kutoka Misri.
“Maandalizi yanaendeelea vizuri na mpaka sasa niko sawa, niwaombe Watanzania na mashabiki wangu kwa ujumla dua zenu zinahitajika na nina imani sitaweza kuuwaangusha, nitawapa shoo-shoo, nina imani sijawahi kuwaangusha, naamini nitafanya vizuri kwa uwezo wa Mungu,” alisema Kiduku.
Naye kocha wa bondia huyo, Pawa Iranda amesem mashabiki wasiwe na wasiwasi kwani kazi yao wanaiamini na huwa haiharibiki huku akisisitiza kuwa kila bondia atakayekuja Tanzania kucheza na Kiduku lazima ashindwe na hiyo ni kutokana na kumuamini Kiduku na maandalizi wanayoyafanya.
Ngumi Kiduku aahidi kutowaangusha Watanzania
Kiduku aahidi kutowaangusha Watanzania
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
