Barcelona, Hispania
Mshambuliaji wa Barcelona, Pierre-Emerick Aubameyang anakamilisha taratibu za kurudi kwenye Ligi Kuu England kujiunga na Chelsea baada ya klabu hizo mbili kufikia makubaliano ya awali ambapo Chelsea inatarajia kutoa kitita cha Pauni 12 milioni pamoja na beki Marcus Alonso.
Aubameyang ambaye alijiunga na Barcelona akitokea Arsenal Januari mwaka huu, hadi sasa ameifungia timu hiyo jumla ya mabao 13 katika mechi 24 na msimu huu umeonekana kuwa mgumu kwake kwani hadi sasa amecheza dakika nane tu.
Aubameyang ambaye ana umri wa miaka 33 anakuwa mchezaji wa saba kusajiliwa na Chelsea, wengine wakiwa ni Wesley Fofana, Raheem Sterling, Cesare Casadei, Kalidou Koulibaly, Carney Chukwuemeka na Marc Cucurella.
Usajili wa Aubameyang katika klabu ya Chelsea unamaanisha kwamba mwenyekiti na mmiliki wa klabu hiyo, Todd Boehly atakuwa katika usajili wake wa kwanza ametumia jumla ya Pauni 250 milioni tangu ainunue klabu hiyo kutoka kwa bilionea wa Urusi, Roman Abramovich.
Aubameyang kwa sasa anasumbuliwa na majeraha ya taya baada ya kuvamiwa na majambazi waliokuwa na silaha akiwa nyumbani kwake na kumpora vitu kadhaa vya thamani lakini akiwa katika hali hiyo mazungumzo yameendelea ili kuiwahi siku ya mwisho ya usajili ambayo ni leo.
Kimataifa Safari ya Aubameyang Chelsea yaiva
Safari ya Aubameyang Chelsea yaiva
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
