Na mwandishi wetu
Timu ya soka ya Azam leo imeendelea na maandalizi yake ya mwisho kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23 ikijiandaa pia kwa ajili ya mechi maalum ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Zesco ya Zambia.
Azam imerejea nchini jana ikitokea El Gouna, Misri ilikokuwa imeweka kambi ya zaidi ya wiki mbili na sasa inatarajia kukamilisha maandalizi yake hayo kupitia mechi hiyo itakayopigwa Jumapili hii.
Mechi hiyo pia ni kwa ajili ya siku maalum ya Azam waliyoipa jina la Azamka itakayotumika kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wao wapya tisa waliowasajili kwa ajili ya msimu wa 2022/23.
Kocha Mkuu wa Azam, Abdihamid Moallin ameeleza kufurahishwa na matokeo ya mazoezi ya maandalizi waliyoenda kufanya nchini Misri yakiwa yamewapa morali kama benchi la ufundi kwa ajili ya mechi za msimu ujao katika michuano mbalimbali watakayoshiriki.
Ikumbukwe kuwa mbali na Ligi Kuu ya NBC na Kombe la FA, Azam pia itapeperusha bendera ya nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao sanjari na timu ya Geita Gold.
“Kwa ujumla ni kazi kubwa imefanyika, kwa uzito mzuri wa mazoezi na kujitoa kwa hali ya juu kwa wachezaji umekuwa mchakato mzuri kwetu kufanya haya maandalizi na tumefurahishwa sana na kazi iliyofanyika kwa muda tuliokuwa Misri,” alisema Moallin.
Soka Azam yajinoa kuikabili Zesco
Azam yajinoa kuikabili Zesco
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
