Na mwandishi wetu
Taifa Stars leo imeibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Somalia kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan).
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Stars ilipata bao hilo pekee dakika moja baada ya kuanza kipindi cha pili mfungaji akiwa ni Abdul Sopu, mchezaji wa zamani wa Coastal Union ya Tanga ambaye hivi karibuni alisajiliwa na Azam FC.
Sopu, mchezaji aliyejipatia umaarufu akiwa Coastal, alifunga bao hilo akiitumia vizuri krosi ya Kibwana Shomari na kuandika bao hilo ambalo licha ya juhudi za Somalia kutaka kusawazisha na Stars kutaka kuongeza lakini hadi filimbi ya mwisho inapulizwa matokeo yalibaki hivyo hivyo.
Timu hizo zinatarajia kurudiana kati ya Julai 29 na 31 na baada ya hapo iwapo itaendeleza ushindi, Stars itaingia raundi ya pili ambapo inatarajia kuumana na Uganda katika mechi itakayochezwa kati ya Agosti 26 na 28 kwa Stars kuanzia nyumbani na kumalizia ugenini kati ya Septemba 2 hadi 4.
Stars: Aishi Manula, Kibwana Shomari, Mohammed Hussein, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Yassin Mzamiru, Abdul Sopu, Salum Abubakar, George Mpole, Feisal Salumu na Kibu Dennis.
Mechi nyingine za Chan kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zilizochezwa leo ni kati ya Ethiopia na Sudan Kusini na Burundi na Djibouti.
Kimataifa Stars yaipiga Somalia Dar
Stars yaipiga Somalia Dar
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also