Na mwandishi wetu
Mshambuliaji mpya wa Simba, Moses Phiri ameahidi kuifanyia timu hiyo mambo makubwa msimu ujao ikiwemo kurudisha mataji waliyoyapoteza msimu uliopita.
Phiri ameelezea namna anavyofurahia maisha mapya akiwa na miamba hiyo ya soka Afrika na kambi hiyo pamoja na kukutana na sura mpya zinazomwongezea ari ya kutaka kufanya vizuri ili kurudisha heshima ya Simba.
“Najisikia furaha sana kuwa sehemu ya kikosi cha Simba, nimefurahi kukutana na changamoto mpya lakini kizuri zaidi kambi tuliyopo inatujenga kuhakikisha tunafanya vizuri na kuhakikisha tunakuwa kitu kimoja na kupigania malengo tuliyokusudia,” alisema Phiri.
Phiri ambaye ni raia wa Zambia amekiri kuwa Ligi Kuu ya NBC imekuwa na ushindani mkubwa siku za karibuni lakini kwa namna timu yao ilivyosajili anaamini hakuna kitakachoshindikana sababu wanacheza kwenye klabu kubwa yenye rekodi nzuri kwenye michuano ya kimataifa akiamini mambo yatakaa sawa msimu ujao wa 2022-23.
Phiri aliyesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Zanaco FC ya Zambia ni miongoni wachezaji wapya waliobeba matumaini ya mashabiki wa Simba kutokana na uwezo alionao kwenye ufungaji.
Wekundu hao kwa sasa wamejichimbia kwenye mji wa Ismailia, Misri kujiandaa na msimu ujao baada ya msimu uliopita kushindwa kutetea ubingwa wa ligi, Kombe la Azam (ASFC) na kushindwa kufikia malengo yao kwenye michuano ya klabu Afrika.
Soka Phiri apania kurudisha mataji Simba
Phiri apania kurudisha mataji Simba
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
