London, England
Mchezaji wa zamani wa Man United, Nani amesema kwamba klabu hiyo haitokuwa imefanya jambo sahihi kumuacha Cristiano Ronaldo aondoke huku akisisitia kuwa anaamini mchezaji huyo atabaki katika klabu hiyo ya Old Trafford.
Kauli hiyo ya Nani imekuja wakati huu mchezaji huyo akiwa ametangaza nia yake ya kutaka kuihama timu hiyo huku akionekana kuwekewa ngumu na mabosi wake ambao wamewahi kusema kwamba mchezaji huyo hauzwi na hata Chelsea waliodaiwa kutaka kumsajili nao wamefuta mipango ya kumchukua winga huyo mwenye miaka 37.
Nani ambaye amewahi kucheza na Ronaldo Man United na kwenye timu ya Taifa ya Ureno amesema Ronaldo ni mchezaji muhimu, “Natumaini atabaki Man United, ni mchezaji muhimu na ambaye wakati wote analeta utofauti na naamini yuko katika hali nzuri ya kuisaidia klabu, naamini atafanya hivyo.”
Nani ambaye amejiunga na klabu ya Melbourne Victory ya Australia alisema kwamba amejaribu kuwasiliana kwa simu na mchezaji huyo mwenzake wa zamani lakini hawakuweza kuzungumza, “nilimpigia lakini akaniambia yuko bize sana, tutazungumza wakati mwingine.”
Awali Ronaldo alidaiwa kutaka kuondoka kwa alichodai kwamba ana hofu ya kutofaa katika mfumo wa kocha mpya Erik ten Haag ingawa kuna madai kwamba kuikosa Ligi ya Mabingwa Ulaya ndiyo sababu inayomfanya atake kuhama.
Kocha Ten Haag, ambaye kwa sasa yuko na kikosi cha timu hiyo katika ziara ya maandalizi ya msimu ujao wa 2022/23 katika nchi za Thailand na Australia, alishasema katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari kwamba mchezaji huyo yumo katika hesabu zake na hauzwi.
Kimataifa Nani amtaka Ronaldo abaki Man Utd
Nani amtaka Ronaldo abaki Man Utd
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
