London, England
Viungo wa Chelsea, N’Golo Kante na Ruben Loftus-Cheek wameshindwa kuungana na wachezaji wenzao kwa safari ya Los Angeles, Marekani sababu ikiwa ni chanjo ya corona.
Msafara wa wachezaji na viongozi wa Chelsea umeondoka Jumamosi hii kuelekea Marekani kwa ziara ya kujinoa na msimu wa 2022/23 lakini Kante na Ruben hawamo katika msafara huo kutokana na sheria za Marekani ambazo zinawazuia wasafiri wasio raia wa nchi hiyo ambao umri wao ni zaidi ya miaka 18 kuingia nchini humo kama hawajachanjwa au kutakuwa na wasiwasi wowote kuhusu chanjo zao.
“N’Golo Kante na Ruben Loftus-Cheek hawatasafiri tatizo likiwa ni chanjo ya corona,” ilieleza kwa kifupi taarifa ya Chelsea kuhusu wachezaji hao.
Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel baada ya kupata habari hizo alidai kwamba hakuwa na uhakika kuhusu suala la chanjo kwa wachezaji wake na ingawa yeye alichanja, hawezi kuwalazmisha wachezaji wake kufanya hivyo.
Ikiwa nchini Marekani, Chelsea iliyomaliza Ligi Kuu England msimu wa 2021/22, inatarajiwa kucheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya timu za Club America mechi itakayopigwa Las Vegas Julai 17 na baada ya hapo watashuka tena dimbani Julai 21 dhidi ya Charlotte FC kwenye Uwanja wa Bank of America na siku mbili baadaye wataumana na mahasimu wao wa London, Arsenal mjini Florida.
Wakati Kante na Ruben wakiachwa, wachezaji Ben Chilwell na Callum Hudson-Odoi ambao wamekuwa wakiandamwa na balaa la kuwa majeruhi kwa muda mrefu wamejumuishwa katika safari hiyo pamoja na wachezaji wengine waliotoka kuuzwa kwa mkopo kina Conor Gallagher, Billy Gilmour, Ethan Ampadu na Michy Batshuayi.
Kimataifa Corona yamzuia Kante kuingia Marekani
Corona yamzuia Kante kuingia Marekani
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
