Na mwandishi wetu
Coastal Union imejipanga kikamilifu kuziba mapengo ya wachezaji wake mahiri walioihama timu hiyo, Abdul Suleiman ‘Sopu’ na Victor Akpan.
Wachezaji hao ambao wameonyesha kiwango kikubwa msimu uliomalizika wa 2021/22 wamesajiliwa na klabu maarufu, Sopu akitimkia Azam na Akpan raia wa Nigeria akitua Simba SC.
Mwenyekiti wa Coastal, Steven Mnguto amesema kwamba wanafahamu wamepoteza wachezaji mahiri lakini anashukuru dili hizo zimekwenda vizuri, imemfurahisha kila mhusika na wanashukuru kuona wanapata mafanikio baada ya uvumilivu wa muda mrefu.
“Kuhusu kuziba mapengo yao, si mapengo isipokuwa ni wachezaji wazuri wameondoka na wachezaji bado wapo wengi, kikubwa ni kukubali kuchukua ‘risk’ kwa ajili ya faida kama hizi na kufanya biashara maana mpira ndiyo biashara yetu.
“Sasa kwenye hizi timu nyingine haziko tayari kufanya hivyo kukisubiri kitu au kukaa nacho kwa muda kwa ajili ya kukulipa kwa hiyo tunashukuru mambo yamekamilika vizuri na kila mmoja amefaidika na kilichotokea, na haya ni mafanikio yetu ya uvumilivu kwenye biashara hii,” alisema Mnguto.
Akpan ametua Simba kwa ajili kuboresha eneo la kiungo la timu hiyo ambalo tayari limeondokwa na Rally Bwalya aliyetimkia Amazulu ya Afrika Kusini pia ikielezwa kwamba Thadeo Lwanga anaweza kutolewa kwa mkopo.
Upande wa Sopu yeye baada ya kuonesha kiwango cha kuvutia msimu mzima na kujitutumua kufunga ‘hat-trick’ kwenye fainali ya Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Yanga ilipelekea kuwaniwa na vigogo Simba na Yanga lakini mwishowe Azam ikamnasa kwa kandarasi ya miaka mitatu.
Soka Coastal wasaka mbadala wa Sopu
Coastal wasaka mbadala wa Sopu
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
