Livepool, England
Hatimaye mshambuliaji Mohamed Salah wa Liverpool amekata mzizi wa fitina kuhusu usajili wake baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu wa kuichezea timu hiyo.
Kwa kipindi kirefu, Salah ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Misri na mwenzake, Sadio Mane wa Senegal wamekuwa katika mjadala kuhusu hatma yao wote wakiwa Liverpool kabla Mane hajajiunga na Bayern Munich na kumuacha Salah akiwa hajulikani kama ataondoka au kubaki.
Salah amemaliza msimu wa 2021/22 wa Ligi Kuu England akiwa mfungaji bora na ameiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe la FA na la Ligi huku wakifikia hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kushindwa kutamba mbele ya Real Madrid walioibuka vinara wakati katika Ligi Kuu England walishika nafasi ya pili baada ya kushindwa kwa tofauti ndogo ya pointi na Man City waliotwaa taji hilo.
Hadi sasa Salah ana rekodi ya kuifungia timu hiyo mabao 156 katika mechi 254 akiwa amebakisha mwaka mmoja kabla ya kumalizika mkataba wake na hivyo uamuzi wake wa kusaini mkataba mpya unakuwa faraja kubwa kwa mashabiki wa Liverpool ambao walihofia kumpoteza mchezaji huyo.
“Ni uamuzi mzuri kwetu na uamuzi mzuri kwake, nafikiri sasa ni wetu, hii ni klabu yake kwa sasa, hili ni jambo zuri kwa mashabiki wetu kufurahia zaidi inapofika mwisho wa wiki, nina hakika kutakuwa na sherehe jioni hii kutokana na habari hii,” alisema kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp.
Akizungumzia uamuzi huo, Salah alisema, “Najisikia vizuri na ninafurahia kushinda mataji na klabu hii, ni siku ya furaha kwa kila mtu, tuko katika nafasi nzuri ya kupigania kila kitu.”
Uamuzi wa Salah mwenye umri wa miaka 30 ni jambo zuri katika klabu hiyo hasa baada ya kuondoka kwa Mane, mchezaji mwingine aliyekuwa tegemeo katika timu hiyo ambayo pia imemsajili mshambuliaji aliyekuwa akikipiga Benfica ya Ureno, Darwin Nunez kwa ada ya Pauni 64 milioni.
Kimataifa Salah asaini miaka 3 Liverpool
Salah asaini miaka 3 Liverpool
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
