Refa ni Arajiga tena
Na mwandishi wetu
Mtanange wa fainali ya Kombe la Azam (ASFC) baina ya Coastal Union dhidi ya Yanga, utakaopigwa
kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha keshokutwa, utaamuliwa na mwamuzi Ahmed Arajiga
wa Manyara.
Hii ni mara ya pili, Arajiga anaamua mchezo wa pili wa Yanga wa FA mfululizo baada ya kuamua mechi
yao iliyopita ya nusu fainali dhidi ya Simba na Yanga kushinda kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba, Mwanza.
Pia kwa Arajiga inakuwa fainali yake ya pili mfululizo ya kombe hilo baada ya msimu uliopita
kuchezesha fainali baina ya Simba na Yanga iliyopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma huku
Simba ikiibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0.
Waamuzi wasaidizi wa mchezo huo wa kufunga rasmi msimu wa soka Tanzania Bara 2021/22 ni Frank
Komba na Janeth Balama huku mwamuzi wa akiba akiwa Radhani Kayoko.
