Na mwandishi wetu
Coastal Union itaikabili Yanga katika mechi za hatua ya 32 bora za Kombe la TFF msimu wa 2024-25, mashindano yanayoendeshwa kwa udhamini wa Benki ya CRDB.
Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo iliyopatikana leo Ijumaa, mahasimu wa Yanga, Simba wao wataumana na TMA Stars.
Timu nyingine za Ligi Kuu NBC zilizomo kwenye ratiba ya michuano hiyo ni Namungo FC ambayo itacheza na Kagera Sugar wakati Fountain Gate wataumana na Stand United.
Azam FC wao wataumana na Mbeya City na Mashujaa wataikabili Geita Gold, Cosmopolitan v KMC, Mbeya Kwanza v Mbambali Academy, Mashujaa FC v Geita Gold, Singida BS v Leo Tena, Tabora United v Transit Camp na JKT Tanzania v Biashara United.
Soka Coastal yapewa Yanga Kombe la TFF
Coastal yapewa Yanga Kombe la TFF
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
