Na mwandishi wetu
Nahodha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta amerejea na kuanza mazoezi kwenye kikosi cha timu yake ya Fernerbahce baada ya kumaliza kuitumikia Royal Antwerp ya Ubelgiji.
Samatta ameonakana juzi akianza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa 2022-23 na kikosi cha timu hiyo chini ya kocha, Jorge Jesus raia wa Ureno.
Akiwa na Anterwap iliyomaliza nafasi ya nne msimu huu kwenye Ligi Kuu ya Ubelgiji, Samatta alifanikiwa kufunga mabao matano na kutoa asisti nne katika mechi 27 alizocheza.
Awali, mnamo Januari, 2020 Samatta alisajiliwa na Aston Villa ya England kwa miaka minne na nusu na kuweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza katika Ligi Kuu England na kuweka rekodi ya Tanzania kuwa taifa la 117 kuwa na mchezaji katika michuano hiyo.
Hata hivyo, baadaye alitolewa kwa mkopo Fernebahce mpaka mwisho wa msimu kabla ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Uturuki kumsajili moja kwa moja na kisha nao kumpeleka kwa mkopo Antwerp kwa msimu mzima kabla ya kurejea sasa.
Mchezaji huyo wa zamani wa Simba na TP Mazembe kuelekea mwisho wa msimu uliomalizika hivi karibuni aliwahi kukaririwa akisema: “Sijui kuhusu siku zijazo, hakuna anayejua kuhusu siku zijazo lakini ninachojua ninarejea Fenerbahce kwa mazoezi ya kabla ya msimu mpya na kujiandaa kwa msimu mpya.
Soka Samatta arejea Fernerbahce
Samatta arejea Fernerbahce
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
