Na mwandishi wetu
Kamati ya uchaguzi ya klabu ya Yanga imesogeza mbele zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu za kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa klabu hiyo utakaofanyika Julai 10 mwaka huu.
Taarifa ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Wakili Malangwe Mchungahela iliyopatikana hii leo ilieleza kuwa, zoezi la uchukuaji fomu sasa litafanyika hadi kesho Ijumaa Juni 10 badala ya leo Alhamisi Juni 9 ambayo ilikuwa siku ya mwisho kwa mujibu wa kalenda ya uchaguzi huo.
Sababu ya kuongeza siku moja kwa mujibu wa taarifa hiyo ni kwa kuwa siku ya kwanza ya uchukuaji fomu, Juni 5 ilikuwa siku ya Jumapili ambayo haikuwa siku ya kazi na hivyo kusababisha zoezi zima kuanza Jumatatu yaani Juni 6.
Wakati kamati ikiongeza siku ya kuchukua fomu, nafasi ya rais au mwenyekiti kama ilivyokuwa ikijulikana zamani ambayo kwa sasa inashikiliwa na Dk Mshindo Msola imeonekana kuogopwa kwani hadi sasa wanaodaiwa kuchukua fomu ni Msola anayetetea nafasi hiyo pamoja na mkurugenzi wa uwekezaji wa makampuni ya GSM, Mhandisi Hersi Said.
Katika nafasi ya wajumbe wanaodaiwa kujitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo ni Ayoub Nyenzi aliyewahi kufanya kazi TFF, naibu meya wa jiji, Saad Khimji na mmoja wa wanachama maarufu katika klabu hiyo, Alexander Ngai.
Soka Yanga waongeza siku uchukuaji fomu
Yanga waongeza siku uchukuaji fomu
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
