Dakar, Senegal
Sadio Mane amedhihirisha ubora wake jana kwa kuiwezesha Senegal kuichapa Benin mabao 3-1 katika mechi yao ya kwanza ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon-2023).
Senegal ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo, wakiongozwa na Mane ambaye alifunga mabao yote peke yake (hat trick), waliandika bao lao la kwanza katika dakika ya 10 tu ya mchezo huo lililofungwa kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji mmoja wa Benin kuunawa mpira ndani ya boksi.
Mane kwa mara nyingine akishirikiana na Pope Matar Sarr waliipatia Senegal bao la pili baada ya Mane kufumua shuti ambalo lilizuiliwa lakini baadaye alimalizia kwa kuujaza mpira wavuni na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko Senegal wakiwa mbele kwa mabao mawili.
Juhudi za Benin kutaka bao katika kipindi cha pili zilionekana lakini walikuwa ni Senegal waliopata bao la tatu likifungwa na Mane tena kwa mkwaju wa penalti ambayo ilitolewa baada ya Ismaila Sarr wa Senegal kuangushwa ndani ya eneo la penalti na kipa wa Benin.
Benin waliendelea kupamba lakini juhudi zao zilikatishwa tamaa baada ya nyota wao, Sessi D’Almeida kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Mane. Hata hivyo dakika nne kabla ya mpira kwisha juhudi hizo zilizaa matunda baada Junior Olaitan kuipatia Benin bao pekee la kufutia machozi.
Kimataifa Mane apiga hat-trick, Senegal ikiilaza Benin
Mane apiga hat-trick, Senegal ikiilaza Benin
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
