Vinara wa mchezo wa Taekwondo nchini Tanzania wametamba katika hatua ya 4 ya mashindano ya Afrika Mashariki na kupata ushindi katika michuano iliyofanyika wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.

Mwenyekiti Taekwondo Association(TTA) Club Said Kennedy Said alisema mashindano hayo yalifanyika Nairobi na ni mara ya nne na Tanzania imeibuka mshindi hivyo ni pongezi kwa taifa
Washindi wa mashindano ya TaeKondo kutoka Dar es Salaam ambayo yamefanyika Nairobi nchini Kenya na kufanya Tanzania kuibuka mshindi Afrika Mashariki. Washindi hao ni Moses Mwanyliu(dhahabu), Navraj Singh Mair (2 dhahabu), Arzu Yilmaz(dhahabu), Mehek Kaur Mair(dhahabu 1), Jaiveer Singh Mair (2 fedha), Ali Hamis Ali (fedha 1), Halil Yusuf (1 shaba) na Sedatt yilmaz (1 shaba)

Washindi kutoka Zanzibar ni Maxmillian Kailangana- (dhahabu 1 na fedha 1), Rashid Hamad Khamis – (dhahabu 2), Ibrahim Ali Yussuf (dhahabu) na 1 shaba), Ibrahim Hamad khamis-(fedha 2) na Ali Mohamed Khamis-(shaba).
Tanzania ilipata ujumla medali za dhahabu 9, Medali za fedha 6 na Medali za shaba 4
