London, England
Baada ya kocha wa Arsenal, Mikel Arteta kuwalaumu waamuzi katika mechi yake na Tottenham, safari hii ni zamu ya kocha wa Everton, Frank Lampard ambaye naye amedai kuwa waamuzi hao wameikwaza timu yake katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Brentford.
Everton jana ililala kwa mabao 3-2 mbele ya Brentford, matokeo ambayo yanaiweka timu ya Everton katika wakati mgumu kwenye mbio za kujinasua na janga la kushuka daraja hasa baada ya timu yake kumaliza mechi hiyo ikiwa na wachezaji tisa uwanjani baada ya Branthwaite na Rondón kupewa kadi nyekundu.
Moja ya matukio yaliyomkera zaidi Lampard ni kitendo cha mchezaji wake Richarlison kuvutwa shati na kulalamika lakini mwamuzi hakuchukua hatua yoyote.
“Unapoona jezi inavutwa hiyo ni faulo mahali popote uwanjani,” alisema Lampard na kushangaa ni kwa nini VAR haikutumika katika tukio hilo.
Lampard tayari yuko kwenye uchunguzi wa FA kutokana na kauli alizowahi kuzitoa baada ya timu yake kulala kwa mabao 2-0 mbele ya Liverpool mwezi uliopita.
Kwa kipigo hicho, Everton inakuwa na tofauti ya pointi mbili kati ya timu tatu zilizo chini ya msimamo wa ligi hiyo zikiwa zinahaha kujinasua na janga la kushuka daraja, inashika nafasi ya 16 ikiwa na pointi 36 wakati ligi hiyo ikiwa imebakiza kati ya mechi mbili hadi tatu kwa kila timu.
Kimataifa Lampard naye alaumu waamuzi
Lampard naye alaumu waamuzi
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
