Na mwandishi wetu
Timu ya ya Azam imejinasibu kuwa kwenye kampeni kabambe kuhakikisha inashinda mechi zake 10 mfululizo zinazofuata za Ligi Kuu NBC ili kujiweka sawa kiushindani kwenye msimamo wa ligi.
Kaimu Ofisa Habari wa Azam, Hashim Ibwe ameeleza kuwa kampeni hiyo imeanza kwenye mechi yao iliyopita waliyoifunga Coastal Union mabao 3-2 na kuiendeleza kwenye mechi inayofuata dhidi ya Polisi Tanzania na nyingine.
Azam inayonolewa na Kally Ongala imeshinda mechi saba mfululizo, inashikilia nafasi ya pili baada ya mechi 14 ikiwa na pointi 32 sawa na vinara Yanga walio juu kwa tofauti ya uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
“Si mechi rahisi, ushindi ni mgumu lakini wachezaji wanafahamu tunahitaji ushindi na wamekuwa askari kweli kuhakikisha wanakamilisha majukumu yao ipasavyo lakini lengo ni kushinda mechi 10 mfululizo.
“Tumeanza hili kwenye mechi ya mwisho dhidi ya Coastal na litaendelea kwenye mechi inayofuata na Polisi Tanzania, Kagera Sugar na nyingine kuhakikisha tunapambana kileleni na kuwapa mashabiki kinashostahili, tumedhamiria kukamilisha hii kampeni ya mechi 10 mfululizo,” alisema Ibwe.
Soka Azam yataka ushindi mechi 10
Azam yataka ushindi mechi 10
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
