Doha, Qatar
Kocha wa timu ya England, Gareth Southgate amesema kwamba nahodha na mshambuliaji wa timu hiyo, Harry Kane atakuwa fiti kwa ajili ya mechi dhidi ya Marekani, kesho Ijumaa.
Kane ambaye pia ni mshambuliaji wa Tottenham Hotspur aliumia kiwiko cha mguu mapema kipindi cha pili katika mechi ya kwanza ya England kwenye fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Iran. Katika mechi hiyo iliyochezwa Jumatatu, England ilitoka na ushindi wa mabao 6-2 ingawa Kane alilazimika kutolewa kutokana na maumivu aliyoyapata.
“Harry yuko vizuri, amefanya mazoezi peke yake kwa muda mdogo lakini kiujumla yuko vizuri kwa ajili ya mechi ya Ijumaa (kesho), alifanyiwa vipimo Jumatano (jana) ili kuhakikisha kila kitu kiko vizuri,” alisema Southgate.
Kane, mmoja wa washambuliaji tegemeo wa England hadi sasa ameifungia timu hiyo jumla ya mabao 51 katika mechi 76 akiwa nyuma ya mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Wayne Rooney ambaye amestaafu kuichezea timu hiyo akiwa na mabao 53.
Wakati huo huo Southgate pia alisema kwamba beki wa timu hiyo, Harry Maguire ambaye naye aliumia na kutolewa katika mechi na Iran, kwa sasa anaendelea vizuri.
Kimataifa Kane fiti kuivaa Marekani
Kane fiti kuivaa Marekani
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
