Doha, Qatar
Nahodha wa timu ya Argentina, Lionel Messi amewaambia wachezaji wenzake wa timu hiyo kwamba hawana wa kumlaumu baada ya kipgo cha mabao 2-1 walichokipata jana Jumanne mbele ya Saudi Arabia katika fainali za Kombe la Dunia.
Argentina iliushangaza ulimwengu wa soka baada ya kipigo hicho licha ya kuianza vizuri mechi hiyo na kupata bao katika dakika ya 10 ya mchezo huo lililofungwa na Messi kwa mkwaju wa penalti.
Matokeo hayo yanabaki kuwa jambo kubwa kwa Saudi Arabia kuifunga moja ya timu ambazo kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia ilikuwa ikitajwa kuwa na nafasi kubwa ya kulibeba taji hilo na ikatarajiwa Saudi Arabia itakuwa timu ya kwanza kwao kupata ushindi lakini matokeo yamekuwa tofuati na kwa mujibu wa Messi matokeo hayo ni pigo kubwa kwao.
“Tulitarajia kuanza na pointi tatu ambazo zingetupa utulivu, mambo hutokea kwa sababu ni lazima tujiandae kwa yajayo, ni lazima tushinde na yote hayo yanategemea na sisi wenyewe,” alisema Messi.
“Hatuna wa kumlaumu, tunakwenda kuwa wamoja zaidi, kundi hili lipo imara na tumeonyesha hilo, ni mazingira ambayo hatukuwahi kuyapitia kwa kipindi kirefu, na sasa tunatakiwa kuonyesha kwamba hili ni kundi lililo imara,” alisema.
“Ni kushindwa kunakoumiza, tunatakiwa kuendelea kujiamini, ni lazima tufunge ukurasa huu na kuangalia mbele, ni lazima tujiulize wapi tulikosea, na kuwa na mtazamo chanya na kuweka fikra zetu kwenye mechi yetu na Mexico,” alisema Messi.
Messi, pia alisema si kweli kwamba waliwadharau Saudi Arabia na kuwataka mashabiki maelfu wa Argentina waliosafiri hadi Qatar kuwa kampeni zao kwenye fainali za Kombe la Dunia zitabadilika watakapokutana na Mexico na Poland, “ujumbe wangu kwa mashabiki, wawe na imani na sisi.”
“Tulijua Saudi Arabia ni timu yenye wachezaji wazuri na ambao wanakwenda vizuri na mpira na wanaisumbu safu ya ulinzi mara nyingi, tulilifanyia kazi hilo lakini kidogo tulikuwa na haraka, ni lazima turudi kwenye msingi , ni lazima tufikirie kuhusu yajayo,” aliongeza Messi.
Kocha wa timu ya Saudi Arabia, Herve Renard alisema baada ya mechi hiyo kwamba huenda wachezaji wa Argentina walikosa hamasa.
Kwa upande wake kocha wa Argentina, Lionel Scaloni alikiri baada ya mechi hiyo kwamba kipigo walichokipata ni ni ngumu kukubaliana nacho lakini aliahidi kwamba timu yake iliyo Kundi C itafuzu hatua inayofuata
Argentina ni moja ya timu ambazo zilitajwa kuwa na uwezo wa kubeba taji hilo ikiwa na rekodi ya kucheza mechi 36 bila ya kupoteza hata moja na ndio vinara wa michuano ya Copa America, taji walilolibeba wakiibwaga Brazil na kama wangeshinda mechi na Saudi Arabia wangekuwa na rekodi ya kutopoteza mechi 37 ambayo imewahi kushikwa na Italia.
Kimataifa Messi: Hatuna wa kumlaumu
Messi: Hatuna wa kumlaumu
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
