Doha, Qatar
England na Wales leo Jumatatu zinacheza mechi zao za kwanza za fainali za Kombe la Dunia, mechi ambazo pia zinawaweka mashabiki katika shauku ya kutaka kujua iwapo manahodha wa timu hizo, Harry Kane wa England na Gareth Bale wa Wales watapingana na Fifa na kuvaa vitambaa vya unahodha vyenye ujumbe uliopigwa marufuku.
England itacheza na Iran wakati Wales itacheza na Marekani, mbali na mchuano baina ya timu hizo mpango wa manahodha wa timu hizo na manahodha wengine saba wa nchi za Ulaya, kuvaa vitambaa maalum ni tukio jingine linaloweza kuteka hisia za mashabiki wa soka wanaofuatilia michuano hiyo.
Qatar ambao ni wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia licha ya kusifiwa kwa maandalizi mazuri lakini wamekuwa wakilaumiwa kwa kwenda kinyume na haki za binadamu ikiwamo unyonyaji na vifo vya wafanyakazi wahamiaji pamoja na kuwanyima haki watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Manahodha wa timu hizo nadaiwa wanataka kuvaa vitambaa vyenye ujumbe unaokemea matukio hayo hususan kutetea haki za watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Bado kuna utata iwapo FA itashikilia msimamo wa kumtaka Kane avae kitambaa hicho na kupingana na agizo la Fifa huku ikieleweka wazi kwamba uamuzi huo utamfanya mchezaji huyo apewe kadi ya njano na huenda ukasababisha FA kupigwa faini.
Kwa upande wa Wales, hadi jana jioni walikuwa hawajaamua nini watakifanya na hivyo kutangaza nia yao ya kutaka ufafanuzi kutoka Fifa kabla ya kuamua nini wakifanye.
Fifa tangu juzi Jumamosi tayari walishatoa vitambaa maalum kwa ajili ya manahodha wa timu, vitambaa ambavyo vina ujumbe unaopinga ubaguzi, unaotaka watoto kulindwa, elimu kwa wote pamoja na utunzaji wa mazingira.
Inadaiwa kwamba kampeni kubwa dhidi ya Qatar inachangiwa na chuki zinazotokana na msimamo wa nchi hiyo kupinga mapenzi ya jinsia moja ambayo ni haramu nchini humo jambo ambalo baadhi ya washiriki hasa wale wa nchi za Ulaya hawalikubali.
Kimataifa Kane kupinga agizo la Fifa?
Kane kupinga agizo la Fifa?
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
