Manchester, England
Winga wa Manchester United, Cristiano Ronaldo amewageukia wamiliki wa klabu hiyo Familia ya Glazer akidai kwamba wameigeuza klabu hiyo kama ‘kituo cha kibiashara’ na hawajali lolote kuhusu mambo ya soka.
Ronaldo amekuwa na wakati mgumu msimu huu, hana uhakika wa namba na amewahi kuondolewa katika kikosi cha kwanza katika mechi dhidi ya Chelsea baada ya kususa kuingia uwanjani akitokea benchi katika mechi dhidi ya Tottenham kabla ya baadaye kususa na kutoka uwanjani kabla ya mechi kumalizika.
Akiizungumzia zaidi Familia ya Glazer iliyoanza kuimiliki klabu hiyo mwaka 2005, Ronaldo alisema kwamba hajawahi kukutana na familia hiyo ambayo alisisitiza kwamba inachoangalia ni masuala ya kibiashata, “Manchester ni klabu ya kibiashara, na wanapata pesa kupitia biashara, itakuwa vigumu kwa Manchester kuwa juu kwenye soka katika miaka miwili au mitatu ijayo.”
Mabosi Man United wamekataa kusema lolote kuhusu shutuma hizo za Ronaldo badala yake wamedai kwamba watatoa taarifa baada ya ukweli wote kujulikana. “Akili yetu kwa sasa ni kujiandaa na hatua ya pili ya msimu huu na kuendelea na juhudi zetu, imani na umoja unaojengwa kati ya wachezaji, kocha, maofisa wa klabu na mashabiki,” ilieleza taarifa ya klabu hiyo.
“Kuna mambo ndani ya klabu ambayo hayaisaidii Manchester kufikia kiwango cha juu kama ilivyo kwa City, Liverpool na hata Arsenal kwa sasa, ni mambo yanayotatiza, ni mambo magumu,” alisema Ronaldo.
Kabla ya kuanza kwa msimu huu, Ronaldo alidaiwa kushinikiza kuihama klabu hiyo jambo ambalo halikufanikiwa baada ya kocha Erik ten Hag kudai kwamba bado anamhitaji na baadaye Ronaldo aliikana habari ya yeye kushinikiza kuhama ingawa kwa kinachoendelea sasa ni wazi kwamba huenda akaihama timu hiyo katika dirisha dogo la usajili.
Kimataifa Ronaldo aiponda Familia ya Glazer
Ronaldo aiponda Familia ya Glazer
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
