Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Geita Gold, Saido Ntibazonkiza amesema kwamba wanashukuru kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC, matokeo ambayo yamewawezesha kugawana pointi moja moja na timu hiyo.
Geita ilicheza na KMC majuzi kwenye Uwanja wa Nyankumbu ambapo Saido ndiye aliyeipatia Geita bao la kuongoza katika dakika ya 36 lakini bao hilo halikudumu kwani dakika tano kabla ya timu hizo kwenda mapumziko Waziri Junior aliisawazishia KMC.
Saido alisema kwamba walikutana na timu ngumu licha ya ukweli kwamba hata hali ya hewa ilichangia kuuyumbisha mchezo. “Tulikutana na timu ngumu ambayo pia inapenda kucheza soka la chini hivyo haikuwa mechi rahisi hata kidogo japo na hali ya hewa ilichangia na ndiyo maana tunashukuru angalau kupata pointi moja.”
“Kiukweli tunashukuru Mungu kwa kupata pointi moja maana hali ya hewa haikuwa nzuri na KMC kama inavyofahamika ni miongoni mwa timu nzuri, nafikiri matokeo pia yalichangiwa na kitendo cha wapinzani wetu kutopata nafasi nyingi nzuri,” alisema Saido.
Kwa matokeo hayo, timu hizo zote sasa zinakuwa na idadi ya mechi tatu za ushindi, sare tano na kufungwa tatu, wote wakiwa na pointi 14.
Soka Sare na KMC yamfariji Ntibazonkiza
Sare na KMC yamfariji Ntibazonkiza
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
