Rio de Janeiro, Brazil
Mshambuliaji wa Arsenal, Gabriel Martinelli yumo kwenye kikosi cha Brazil kitakachokwenda Qatar kwenye fainali za Kombe la Dunia wakati Roberto Firmino wa Liverpool ameachwa.
Martinelli ambaye ndio kwanza ana miaka 21, hadi sasa ameifungia Arsenal mabao matano katika mechi 13 alizocheza msimu huu kwenye Ligi Kuu England wakati Firmino hadi sasa ameifungia Liverpool mabao sita katika mechi 12.
Nyota mwingine wa Arsenal, Gabriel ambaye ni beki ameachwa na kuitwa mshambuliaji mwingine wa timu hiyo, Gabriel Jesus ambaye mwezi uliopita hakuitwa kwenye mechi za kirafiki na kuonekana kama vile asingekuwa na nafasi tena katika timu hiyo inayonolewa na kocha Tite.
Katika fainali za Kombe la Dunia, Brazil itarusha karata yake ya kwanza dhidi ya Serbia Novemba 24 kabla ya kuumana na timu nyingine za Kundi G za Cameroon na Switzerland.
Mbali na wachezaji hao, Tite pia amewajumuisha wachezaji wengine wanaocheza England kutoka klabu za Man City, Man United, Newcastle, Liverpool na West Ham.
Kikosi kamili cha wachezaji wa Brazil na timu wanazotoka kwenye mabano ni kama ifuatavyo…
Makipa: Alisson (Liverpool), Ederson (Man City), Weverton (Palmeiras)
Mabeki Dani Alves (UNAM), Danilo (Juventus), Alex Sandro (Juventus), Alex Telles (Sevilla), Bremer (Juventus), Eder Militao (Real Madrid), Marquinhos (PSG), Thiago Silva (Chelsea)
Viungo: Casemiro (Man United), Everton Ribeiro (Flamengo), Bruno Guimaraes (Newcastle), Fabinho (Liverpool), Fred (Man United), Lucas Paqueta (West Ham)
Washambuliaji: Antony (Man United), Gabriel Jesus (Arsenal), Gabriel Martinelli (Arsenal), Neymar (PSG), Pedro (Flamengo), Raphinha (Barcelona), Rodrygo (Real Madrid), Richarlison (Tottenham Hotspur), Vinicius Jr (Real Madrid).
Kimataifa Firmino aachwa Brazil, Martinelli ndani
Firmino aachwa Brazil, Martinelli ndani
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
