Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa timu ya Simba Queens, Charles Lukula amewapongeza wachezaji wake kwa ushindi walioupata wa mabao 2-0 dhidi ya Determine Girls ya Liberia katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo yanafanyika nchini Morocco.
Simba juzi iliandika ushindi wake wa kwanza kwenye michuano hiyo na kupata pointi tatu ambazo zimewaweka katika nafasi ya tatu kwenye Kundi B linaloongozwa na wenyeji AS FAR wenye pointi sita kufuatia kushinda mechi zao mbili za awali.
Lukola raia wa Uganda, ameeleza kuwa wachezaji wake walicheza kwa kujituma na kutimiza ipasavyo majukumu ambayo aliwaelekeza na anafurahi kuona wameyatekeleza kwa asilimia 100.
“Mashindano haya si rahisi kama watu wanavyofikiria, kupata ushindi kumetuongezea nguvu ya kuendelea kupambana kwenye mechi zijazo lakini lazima niwapongeze wachezaji wangu kwa kutimiza vizuri wajibu wao ndani ya uwanja,” alisema Lukula.
Kwa ushindi huo, Queens sasa itamaliza mechi za hatua ya makundi kwa kucheza na Green Buffaloes ya Zambia ambayo ipo nafasi ya pili kwenye kundi hilo wakilingana pointi na Queens lakini miamba hiyo kutoka ukanda wa Cecafa imezidiwa kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa na Wazambia hao.
Queens itaumana na Buffaloes Uwanja wa Novemba 05, Jumamosi hii ukiwa mchezo wa mwisho wa kundi B, ambapo mshindi wa mechi hiyo ataungana na wenyeji AS FAR kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Soka Kocha Simba Queens awapongeza wachezaji
Kocha Simba Queens awapongeza wachezaji
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
