Manchester, England
Mshambuliaji wa Man United, Marcus Rashford amesema kwa sasa fikra zake hazipo kwenye fainali za Kombe la Dunia badala yake anachowaza ni kuipigania timu yake katika top four kwenye Ligi Kuu England.
Rashford ambaye jana Jumapili aliifungia Man United bao la ushindi dhidi ya West Ham ameng’ara katika siku za karibuni na klabu hiyo jambo ambalo linampa nafasi kubwa ya kuwamo kwenye kikosi cha England kitakachokwenda Qatar kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza kutimua vumbi Novemba 20.
Wakati mzuka wa fainali hizo ukionekana kupanda kwa wachezaji wengi, Rashford mwenye umri wa miaka 25 amesema kwamba akili yake haipo kwenye michuano hiyo na badala yake anaziwaza mechi zilizobaki za Man United kabla ya kwenda Qatar kwenye fainali za Kombe la Dunia. “Sifikirii fainali za Kombe la Dunia hata kidogo,” aliongeza Rashford.
“Nafikiria mechi ijayo, ni lazima tuwe tunashinda mechi zetu hapa, bado tuna mechi mbili za ligi kabla ya Kombe la Dunia kama tutashinda mechi hizo mbili tutakuwa vizuri katika mbio za top four, kwa hiyo hicho ndicho ninachokifikiria,” alisema.
Mabao mawili ambayo Rashford amefunga dhidi ya timu za FC Sheriff na West Ham yote ameyafunga kwa mipira ya kichwa jambo ambalo kocha wa Man United, Erik ten Hag amesema mchezaji huyo alikuwa akilifanyia juhudi kwenye mazoezi.
“Kuufuata mpira wa juu ni jambo moja lakini mbinu na shauku ya kutaka kukifikisha kichwa chako eneo husika hilo ndilo jambo ambalo nimekuwa nikilifanyia kazi, ni jambo zuri kufunga mabao kadhaa ya aina ile,” alisema Rashford.
Kimataifa Rashford awaza top four, si Kombe la Dunia
Rashford awaza top four, si Kombe la Dunia
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
