London, England
Brighton, Jumamosi hii imeishangaza Chelsea kwa kuichapa mabao 4-1 katika Ligi Kuu England, matokeo ambayo yamemfanya kocha wa Chelsea, Graham Potter aliyekuwa akiinoa Brighton hapo kabla kujikuta akizomewa na mashabiki wa timu yake ya zamani.
Brighton ilipata bao lake la kwanza katika dakika ya tano lililofungwa na Leandro Trossard kabla ya kuneemeka na mabao mawili ya kujifunga ya Ruben Loftus-Cheek dakika ya 14 na Trevoh Chalobah dakika ya 42 na kwenda mapumziko Brighton ikiwa mbele kwa mabao 3-0.
Chelsea, waliokuwa ugenini jana walikianza kwa kasi kipindi cha pili wakionekana kudhamiria kupindua matokeo na kupata bao la kwanza dakika ya 48 lililofungwa na Kai Havertz na kuanza kuwasakama Brighton ambao safu yao ya ulinzi na kipa Robert Sanche walikuwa imara kudhibiti mashambulizi kabla ya kuandika bao la nne katika dakika za nyongeza lililofungwa na Pascal Grob.
Huo ni ushindi wa kwanza kwa Brighton kuifunga Chelsea katika mechi ya ligi na unamuachia maswali mengi Potter ambaye jana alikuwa akifikisha siku ya 52 tangu aondoke katika timu hiyo na kujiunga na Chelsea akichukua nafasi ya Thomas Tuchel aliyetimuliwa kutokana na matokeo mbaya wa timu hiyo.
Kwa Potter hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza dhidi ya timu yake ya zamani, mechi ambayo matokeo yake yameivuruga rekodi aliyoanza kujiwekea katika timu ya Chelsea ya kutopoteza mchezo katika mechi tisa za michuano mbalimbali.
“Ndio ni kweli kwamba matokeo na kufungwa ni jambo linaloumiza, bado hatujakaa sawa, mara baada ya mashabiki kutusakama hali ikawa ngumu kwetu, Brighton walikuwa na mchezo mzuri hususan kipindi cha kwanza,” alisema Potter.
Kuhusu mapokezi mabaya aliyoyapata kwenye timu yake ya zamani kwa namna mashabiki wa Brighton walivyokuwa wakimzomea kwa kumtaja jina lake mara kwa mara na kumtaka asome matokeo, Potter alisema, “sina cha kusikitika, watu wana uhuru wa kuwa na mawazo yao, nafikiri nilifanya kazi nzuri katika klabu na kuiacha ikiwa katika nafasi nzuri.”
“Kilichotokea ni sehemu ya mchakato, ni lazima utaabike na kusikia maumivu ili ukomae na kuwa bora, hakuna aliyesema kwamba tumefika mwisho, ni lazima tuyachukue maumivu ya leo (jana Jumamoi) na kujifunza,” alisema.
Tangu Potter aondoke Brighton timu hiyo imeshindwa kupata ushindi katika mechi tano na bila shaka matokeo ya mechi dhidi ya Chelsea yanaweza kuwa mwanzo mpya wa ushindi katika timu hiyo.
Matokeo ya mechi za EPL wikiendi hii…
Leicester 0-1 Man City
Bournemouth 2-3 Tottenham
Brentford 1-1 Wolves
Brighton 4-1 Chelsea
Crystal Palace 1-0 Southampton
Newcastle 4-0 Aston Villa
Fulham 0-0 Everton
Liverpool 1-2 Leeds
Kimataifa Potter azomewa Chelsea ikilala 4-1
Potter azomewa Chelsea ikilala 4-1
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
