Na mwandishi wetu
Timu ya soka ya Wanawake ya Simba Queens, imesema hakuna timu wanayoihofia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayotarajiwa kuanza kuunguruma nchini Morocco hivi karibuni.
Akizungumzia maandalizi yao, kipa wa timu hiyo, Gelwa Yona alieleza namna gani watu wamekuwa wakiwaona kama wageni na wanaenda kujifunza lakini yeye anaamini wana nafasi ya kufanya vizuri na kuwashangaza wengi.
“Tunaendelea na maandalizi mazuri kuhakikisha tunaenda kufanya vizuri, naamini timu yetu iko vizuri na kuna kitu tutaenda kufanya, tutawashangaza kwa sababu wengi wanahisi sisi ni wageni hivyo hatutaonesha kitu,” alisema Gelwa.
Kwenye michuano hiyo inayotarajia kuanza kutimua vumbi Oktoba 30 mpaka Novemba 13, mwaka huu, Simba imepangwa Kundi A dhidi ya wenyeji AS FAR, Green Buffaloes ya Zambia na Determine Girls kutoka Liberia.
Kundi B linaundwa na timu za Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Bayelsa Queens (Nigeria), Wadi Degla (Misri) na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya wanawake ya Wekundu hao kuiwakilisha nchi kwenye michuano hiyo iliyoanza rasmi msimu uliopita na Mamelodi kutwaa ubingwa huo kwa kuifunga Hasaacas Ladies ya Ghana mabao 2-0 kwenye fainali iliyopigwa mjini Cairo, Misri.
Soka Simba Queens full kujiamini
Simba Queens full kujiamini
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
