London, England
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amekutwa na hatia na FA baada ya kutolewa nje wakati wa mechi ya timu yake dhidi ya Man City ambayo Liverpool ilishinda kwa bao 1-0.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England iliyochezwa Jumapili, Klopp alitolewa nje kwa madai ya kumtolea maneno makali mwamuzi msaidizi kwa kumsogelea sikioni kwa kile kilichomkera kwa kitendo cha Mohamed Salah kuchezewa rafu lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Klopp amepewa hadi keshokutwa Ijumaa kujibu tuhuma zinazomkabili ingawa leo Jumatano anatarajia kuwapo kwenye benchi la Liverpool wakati timu yake ikiwa nyumbani kuikabili West Ham.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Klopp aliomba radhi, “Kuna jambo limejitokeza katika mazingira hayo, sijivunii jambo hilo hata kidogo, ilikuwa sahihi mimi kupewa kadi nyekundu, na kwa namna ambavyo naliangalia jambo lile kwa wakati huu, haikuwa sahihi.”
Taarifa ya FA ilieleza kuwa Klopp amekutwa na hatia ya kuvunja kanuni ya FA inayohusu kutoa kauli ambazo si sahihi na ambazo zinaweza kuuingiza mchezo wa soka katika vurugu kwa kutoa kauli za kutisha, kukosa uungwana na kutusi.
Baada ya mechi hiyo, Klopp alisema kwamba alikwenda kuonana na mwamuzi Anthony Taylor na kuzungumza naye taratibu kuhusu tukio hilo na namna lilivyokuwa. “Ilikuwa ni mechi iliyojaa ushindani na maamuzi mengi ambayo hatukuyaelewa kwa pande zote mbili, sifurahii nilichokifanya lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa na kila mtu aliona.” aliongeza Klopp.
Kimataifa FA yajiandaa kumuadhibu Klopp
FA yajiandaa kumuadhibu Klopp
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
