Na mwandishi maalum
Timu ya soka ya wasichana chini ya miaka 17 ya Tanzania, Serengeti Girls leo imepata ushindi wake wa kwanza wa mabao 2-1 kwenye fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini India.
Serengeti ambayo ni timu ya kwanza ya soka ukiacha ile ya walemavu, kufuzu fainali za Kombe la Dunia kwa Tanzania, iliibuka na ushindi huo baada ya kuanza vibaya mechi yao ya kwanza ya Kundi D kwa kufungwa mabao 4-0 na Japan.
Katika mechi ya leo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Nehru, Serengeti iliandika bao la kwanza katika dakika ya 17 mfungaji akiwa ni Diana Mnally ambaye aliyatumia makosa ya safu ya ulinzi ya Ufaransa kuuzuia vizuri mpira wa kona kwenye lango lao.
Christer Bahera aliifungia Serengeti bao la pili katika dakika ya 60 wakati bao pekee la Ufaransa lilipatikana katika dakika ya 77 lililofungwa na Lucie Calba kwa mkwaju wa penalti.
Serengeti hata hivyo ilipata pigo na kulazimika kubaki na wachezaji 10 uwanjani baada ya Joyce Lema kutolewa kwa kadi nyekundu (mbili za njano) na hivyo atakosa mechi ya tatu ya Serengeti dhidi ya Canada itakayochezwa Jumanne.
Kimataifa Serengeti Girls yatamba Kombe la Dunia
Serengeti Girls yatamba Kombe la Dunia
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
