Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Ihefu FC, Juma Mwambusi ametamba kuwa paoja na timu yake kuwa katika mwenendo wa kusuasua lakini haitoshuka daraja na kuwataka wale wote wanaoiombea mabaya wasahau hilo.
Timu hiyo ipo mkiani mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi moja iliyoipata juzi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons.
Kocha huyo amekiri ligi ya msimu huu kuwa ngumu ukilinganisha na misimu iliyopita lakini hicho siyo kisingizio cha kufanya washindwe kupata matokeo mazuri kwenye mechi zao kama ilivyo timu nyingine.
“Presha imekuwa kubwa kwetu kutokana na mtiririko wa matokeo ya kufungwa mechi nne mfululizo lakini niwaambie tu watu huu ni mpira vitu kama hivi vinatokea, hata kwa klabu kubwa. Kitu kizuri kwa Ihefu kimejitokeza mapema mwanzoni mwa msimu naamini kitapita na tutashinda na kubaki ligi kuu msimu ujao,” alisema Mwambusi.
Mwambusi aliyewahi kuzinoa Yanga na Mbeya City, amefafanua kuwa kitu kinachompa matumaini ni kazi aliyoianza tangu akabidhiwe mikoba ya kuinoa timu hiyo imeanza kuonekana kuanzia mabadiliko ya kiuchezaji na uwajibikaji wa wachezaji ndio maana wakapata hiyo pointi moja.
Kocha huyo pia amesema kwamba yeye na wachezaji wake hawajakata tamaa, wanaendelea kupambana kuipigania timu yao kuhakikisha wanarudi kwenye mstari na kuondoka kwenye nafasi mbaya waliyopo sasa na kukwea nafasi za juu.
Soka Ihefu haishuki daraja-Mwambusi
Ihefu haishuki daraja-Mwambusi
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
