Na mwandishi wetu
Kocha wa timu ya soka ya taifa chini ya umri wa miaka 23, Hemed Selamani ‘Morocco’ amewatuliza mashabiki baada ya kutoka suluhu dhidi ya Sudan Kusini katika mchezo wa kufuzu fainali za Afrika akisema atarekebisha mapungufu kwa ajili ya kufanya vizuri.
Katika mchezo huo wa kwanza uliochezwa majuzi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, timu hiyo haikufanikiwa kupata ushindi kutokana na uimara wa timu pinzani.
Akizungumza baada ya mchezo huo Morocco alisema kwamba wachezaji wengi alionao ni wapya, timu ni ngeni kwake lakini tayari amewaona na wanajipanga kurekebisha mapungufu kufanya vizuri michezo inayokuja.
“Kwangu mimi hii ni timu mpya ndiyo kwanza nimewaona wachezaji, tutajipanga kwa mchezo ujao naamini tutashinda, tunarudi kwenye ubao kwa siku chache zilizobaki kuhakikisha uwanjani tunafanya vizuri na kupata matokeo,” alisema.
Morocco alisema katika mchezo huo walishindwa kupata matokeo kwa sababu walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani na wachezaji walicheza kwa presha ya kutaka matokeo mazuri.
Alisema kipindi cha kwanza hawakucheza vizuri na wapinzani walikuwa wanacheza zaidi katika eneo lao kwa ajili ya kulinda kiasi cha wachezaji wake kushindwa kupenya japo kipindi cha pili walijaribu kubadilisha mfumo na wachezaji wake ila bado milango ya wapinzani ilikuwa migumu.
Tayari kikosi hicho kimeshaondoka nchini kuelekea Rwanda kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayopigwa nchini humo leo Jumatatu jioni.
Soka Morocco awatuliza mashabiki
Morocco awatuliza mashabiki
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
