Milan, Italia
England imechapwa bao 1-0 na Italia katika mechi ya Uefa Nations Ligi iliyopigwa Ijumaa hii, matokeo ambayo pia yanazidi kumuweka pabaya kocha wa timu hiyo, Gareth Southgate ikiwa imebaki takriban miezi miwili kabla ya fainali za Kombe la Dunia.
Matokeo hayo ni mwendelezo wa matokeo yasiyo ya kuvutia ya England hali ambayo imeanza kuibua wasiwasi kuhusu ushiriki wa timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia kwani tayari Southgate ameanza kutupiwa lawama yeye na wachezaji wake.
Kocha huyo ambaye amekiri kwamba lawama dhidi ya timu yake anazikubali na haziepukiki huenda akatangaza kikosi cha England wakati wowote baada ya mechi ya Jumatatu dhidi ya Ujerumani huku mwenendo wa timu ukizidi kuwachanganya mashabiki kwa kuwa unazidi kufifisha matumaini ya timu yao kufanya vizuri kwenye Kombe la Dunia.
Bao pekee la Italia katika mechi hiyo lililofungwa na Giacomo Raspadori katika dakika ya 68 limeiweka England mkiani katika kundi lake ambalo pia lina timu za Hungary inayoshika usukani ikifuatiwa na Italia na Ujerumani.
Timu ya England hadi sasa haijashinda hata mechi moja na wala haina bao lolote katika mechi zao tano zilizopita matokeo ambayo yamezidisha hasira za mashabiki waliosafiri hadi Milan kwa ajili ya mechi hiyo ambao waliamua kumalizia hasira zao kwa kumzomea kocha huyo wakati akitoka uwanjani.
Southgate hata hivyo aliishia kusema kwamba yuko tayari kupokea lawama hizo.
Akiuzungumzia mchezo ulivyokuwa kiungo, Declan Rice alisema kwamba timu ya England ilicheza chini ya kiwango ingawa alidai kwamba waliutawala mchezo.
“Sidhani kama mambo ni mabaya sana, tulikuwa vizuri, ni kiwango walau bora kidogo ukilinganisha na siku za nyuma, si kwamba hatukuwa tukitengeneza nafasi, kuna mabao kwa ajili ya mashabiki, niamini mimi katika hilo, tutakuwa vizuri tu.”
Matokeo ya mechi za Uefa Nations Ligi ni kama ifuatavyo
Italia 1-0 England
Ujerumani 0-1 Hungary
Georgia 2-0 North Macedonia
Bulgaria 5-1 Gibraltar
Estonia 2-1 Malta
Ujerumani 0-1 Hungary
Italia 1-0 England
Bosnia-Herzegovina 1-0 Montenegro
Finland 1-1 Romania
Mechi za leo za Uefa Nations Ligi
Ireland Kask v Kosovo
Scotland v R. of Ireland
Armenia v Ukraine
Slovenia v Norway
Cyprus v Ugiriki
Czech Rep v Ureno
Spain v Switzerland
Israel v Albania
Serbia v Sweden
Kimataifa England yamuweka pabaya Southgate
England yamuweka pabaya Southgate
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
