London, England
Klabu ya Brighton imemteua kocha wa zamani wa Shakhtar Donetsk, Roberto De Zerbi kuchukua nafasi ya Graham Potter aliyehamia Chelsea.
De Zerbi, kocha Mtaliano tayari amesaini mkataba wa miaka minne, kabla ya hapo kocha huyo aliwahi kuinoa klabu ya Sassuolo ya Serie A nchini Italia na kumaliza nayo msimu wa 2020/21 katika nafasi ya nane kabla ya kutimkia Ukraine alipojiunga na Shakhtar Donetsk.
“Hakika nimefurahi Roberto amekubali kuwa kocha wetu mkuu mpya, timu ya Roberto inacheza soka zuri na lenye kuvutia na soka linaloonyesha ujasiri na naamini staili yake na mbinu anazotumia zitafaa katika kikosi tulichonacho,” alisema Mwenyekiti wa Brighton, Tony Bloom.
De Zerbi mwenye miaka 43, anachukua nafasi ya Potter ambaye amejiunga na Chelsea mapema mwezi huu baada kuinoa Brighton kwa misimu mitatu yenye mafanikio ambayo ndiyo yaliyowashawishi matajiri wa Chelsea kumchukua baada ya klabu hiyo kuachana na kocha Mjerumani, Thomas Tuchel.
Brighton kwa sasa inashika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu England ikiwa na pointi 13 baada ya mechi sita na mtihani wa kwanza kwa kocha huyo katika Ligi Kuu England utakuwa ni Oktoba Mosi dhidi ya Liverpool.
Kimataifa Mtaliano amrithi Potter Brighton
Mtaliano amrithi Potter Brighton
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
