London, England
Sare ya bao 1-1 iliyoipata Chelsea Jumatano usiku katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Red Bull Salzburg si matokeo mazuri kwa timu iliyobeba taji msimu wa 2020/21 lakini kocha wao mpya, Graham Potter ambaye hiyo ni mechi yake ya kwanza kwenye ligi hiyo amewatetea wachezaji wake.
Matokeo hayo japo yanawafariji Chelsea baada ya kulala kwa bao 1-0 katika mechi ya awali dhidi ya Dinamo Zagreb wakati timu hiyo ikinolewa na Thomas Tuchel aliyetimuliwa, yanaifanya Chelsea kuwa mkiani mwa Kundi E huku ikijiandaa kuikabili AC Milan katika mechi ijayo.
Kwa maana nyingine haitoshangaza kwa Potter kuonja ladha ya Ligi ya Mabingwa katika hatua ya makundi pekee jambo ambalo huenda likazidisha hasira ya mashabiki wa Chelsea ambao walionekana kushangazwa na uamuzi wa vigogo wa klabu hiyo kumfuta kazi kocha mwenye taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kumpa kazi hiyo kocha ambaye mafanikio pekee aliyonayo Ulaya ni kwenye hatua ya 32 bora ya Europa Ligi wakati akiwa na timu ya Ostersunds ya Sweden.
Potter hata hivyo kwa upande alisema anajivunia wachezaji wake kwa namna walivyompokea vizuri kocha mpya mwenye mipango mipya.
“Tumechanganywa kwa kupata pointi moja lakini nafikiri wachezaji wameichukulia vizuri mechi hii, wamejitoa kwa kila kitu na najivunia kwa walichofanya leo (jana),” alisema.
“Haikuwa rahisi kwao, unajua mabadiliko ya kocha na yote hayo yanakuja na mambo mapya lakini wamekabiliana na hali hiyo vizuri, walionyesha kuwa profesheno, walitulia na kuwajibika, kwa hiyo katika suala zima la kujitolea walikuwa sawa kwa silimia 100,” alisema.
Matokeo ya Jumatano hii ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kama ifuatavyo…
Rangers 0-3 Napoli
AC Milan 3-1 Dinamo Zagreb
Chelsea 1-1 Red Bull Salzburg
Shakhtar Donetsk 1-1 Celtic
Real Madrid 2-0 RB Leipzig
FC Copenhagen 0-0 Sevilla
Man City 2-1 Borussia Dortmund
Juventus 1-2 Benfica
Maccabi Haifa 1-3 PSG
Kimataifa Potter awatetea wachezaji Chelsea
Potter awatetea wachezaji Chelsea
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
