Na mwandishi wetu
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) , Neema Msitha amewaomba Watanzania kupuuza taarifa ya Rais wa Shirikisho la Soka kwa wenye ulemavu Tanzania (TAFF), Peter Sarungi, anayedai kuwa tangu kufungiwa kwake, maandalizi ya timu hiyo hayakwenda vizuri jambo ambalo halina ukweli.
Msitha alisema Sarungi pamoja na viongozi wengine wa TAFF walisimamishwa kujihusisha na kambi ya timu ya watu wenye ulemavu kutokana na tuhuma za kuwanyanyasa wachezaji.
“Sarungi na wenzake walisimamishwa kwa kipindi fulani, wakaendelea na shughuli nyingine za chama lakini sio kuwa sehemu ya kambi ya timu ya taifa hata hivyo baraza limesikitishwa na tuhuma zake za uongo na ubinafsi kwa serikali kutokana na yeye kusimamishwa kwa makosa yake binafsi ndiyo akazusha uzushi huo.
“Inaeleweka wazi Rais Samia Suluhu Hassan, alielekeza timu hii ipewe maandalizi ya kutosha na timu hii imekaa kambini tangu mwezi Februari, hivi sasa timu inaelekea nchini Uturuki kuendelea na kambi yake.
“Kwa kuwa timu imekaa kambini Tanzania kwa muda mrefu tumeona iende kuweka kambi nchini Uturuki kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa na mazingira ya nchini humo lakini ikumbukwe timu hiyo ilipelekwa nchini Poland kushiriki mashindano ikiwa ni muendelezo wa kushiriki mashindano haya,” alisema Msitha.
Aidha, imeelezwa kuwa BMT inachukua hatua zaidi za kinidhamu na kukamilisha jalada la tuhuma zake ikiwemo kupeleka taarifa potofu ili kuhujumu ushiriki wa nchi, hivyo Watanzania wanaombwa kumpuuza na kuendelea kuiombea na kuipa msaada Tembo Warriors, ikaiwakilishe nchi katika Kombe la Dunia nchini Uturuki, Oktoba, mwaka huu.
Sports Mix BMT yataka kigogo TAFF apuuzwe
BMT yataka kigogo TAFF apuuzwe
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
