Barcelona, Hispania
Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Barcelona au Barca, Jordi Cruyff amesema jiji la Barcelona liko moto kwa mara nyingine baada ya klabu hiyo kusajili wachezaji ambao wameamua kufuata ndoto zao badala ya pesa.
Msimu uliopita ulikuwa mgumu kwa Barca ambayo ilijikuta katika deni la Pauni bilioni 1.15 hali ambayo iliwafanya kumruhusu mshambuliaji wao nyota Lionel Messi kujiunga na klabu ya Paris St-Germain (PSG) akiwa mchezaji huru.
Matatizo ya klabu hiyo ya nje ya uwanja na udhaifu wa timu yao uliwafanya wasitoe upinzani wa kutosha kwa Real Madrid ambao walibeba taji la La Liga pamoja na lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.
Katika kinachoonekana kuwa mambo hayakuwa mazuri, matokeo hayo yanakuwa ni mara ya kwanza kwa Barca kumaliza kipindi cha miaka mitatu bila ya kubeba taji la ligi tangu hali hiyo ijitokeze katika msimu wa 2003-04.
Katika kukabiliana na hali hiyo, Barca imefanikiwa kufanya usajili mpya katika majira ya kiangazi wakiwamo Robert Lewandowski, Raphinha na Jules Kounde.
“Barcelona imekuwa tamu,” alisema Cruyff akiwa na mtaalam wa soka nchini Hispania, Guillem Balague kabla ya kufanyika kwa mkutano maalum wa Cruyff Legacy ambapo magwiji wa soka akiwamo Arsene Wenger, Ronald Koeman na Sarina Wiegman wanatarajiwa kuwasilisha mada.
“Unaweza kuona hali ya kujivunia katika macho ya wachezaji wnaapopata nafasi ya kusajiliwa na Barcelona na hilo limekuwa likisaidia sana, kuwa tayari kushindana na klabu zenye bajeti kubwa na mishahara mikubwa.”
“Walitaka kusajiliwa na Barcelona na tunawashukuru wachezaji hawa kwa sababu, niamini mimi walikuwa na ofa kubwa kuliko sisi lakini bado wakaamua kufuata ndoto zamabo, kuwa sehemu ya historia , unapoona macho yanang’ara kwa wachezaji hawa unajua upo katika sehemu maalum.”
Hadi sasa Barca haijapoteza mchezo wowote msimu huu na kikosi hicho kinachonolewa na kocha Xavi kimeshatoa kipigo cha mabao 5-1 katika mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Viktoria Plzen Jumatano iliyopita.
Kimataifa Barca yarudisha utamu Barcelona
Barca yarudisha utamu Barcelona
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
