Na mwandishi wetu
Meneja wa klabu ya Simba, Patrick Rweyemamu amesema mechi mbili ambazo timu hiyo imecheza nchini Sudan zimekiimarisha kikosi chao na sasa wapo tayari kwa mapambano katika michuano yote wanayoshiriki.
Simba ilikuwa nchini Sudan kwa mwaliko wa klabu ya Al Hilal ambapo walicheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya Asante Kotoko na kushinda mabao 4-2 na mchezo wa pili walicheza jana na wenyeji wao ambapo walipoteza kwa bao 1-0.
Patrick ameeleza kuwa mechi hizo mbili zimemsaidia kocha wao Zoran Maki, kujua uwezo wa wachezaji wake hasa wale ambao hajapata nafasi ya kuwatumia katika mechi za Ligi Kuu ya NBC.
“Simba tunaishukuru klabu ya Al Hilal kwa mwaliko waliotupa, ukweli wametusaidia kukiimarisha kikosi chetu kuelekea michuano ya kimataifa lakini pia imempa nafasi kocha kuwajua vizuri wachezaji ambao hajawahi kuwatumia kwenye mechi za ligi.
“Ni ushindani mkubwa tumekutana nao huku, umetusaidia mno katika mechi hizi mbili tulizocheza Sudan ambazo zimetupa uhalisia wa namna tulivyoimarika kuelekea kwenye mbio za michuano tunayoshiriki msimu huu,” alisema Patrick.
Simba sasa imebakisha mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya AS Arta ya Djibouti watakaocheza Dar es Salaam Agosti 3 kabla ya kurejea kwenye Ligi Kuu kuvaana na KMC mnamo Septemba 7 na baada ya hapo itavaana na Nyasa Big Bullets ya Malawi katika mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Septemba 10, mwaka huu.
Soka Simba: Mechi za kirafiki zimetuimarisha
Simba: Mechi za kirafiki zimetuimarisha
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
