Na mwandishi wetu
Mshambuliaji mpya wa timu ya Al-Qadsiah FC, Simon Msuva ameanza vyema baada ya juzi kufunga bao la kwanza katika mechi yake ya kwanza ya ligi akiwa na timu hiyo dhidi ya Al-Akhdoud.
Msuva alifunga bao hilo la kufutia machozi baada ya timu hiyo kulala kwa mabao 3-1 katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Ligi Daraja la Kwanza Saudi Arabia, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Prince Saud.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars aliweka bao hilo kimiani kwa kichwa akiunganisha mpira mrefu uliopigwa kutoka pembeni ya uwanja na kuyafanya matokeo kuwa 2-1 kabla ya baadaye wapinzani wao kuongeza bao la tatu.
Katika kudhihirisha furaha ya kuanza vizuri, Msuva aliweka kipande cha video ya bao hilo na kuandika: “Mechi ya kwanza ya msimu, bao la kwanza la msimu.”
Msuva aliyewahi kuitumikia Yanga na Moro United amejiunga na Al-Qadsiah kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuvunja mkataba wake na mabingwa wa Afrika, Wydad Athletic kutokana na kuidai klabu hiyo malimbikizo ya mishahara pamoja na fedha za usajili.
Hata hivyo, Julai mwaka huu Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) liliimaliza kesi hiyo kwa kuiagiza Wydad kumlipa Msuva Dola za Marekani 700,000 (zaidi ya Sh 1.6 bilioni).
Kimataifa Msuva aanza kutupia Al-Qadsiah
Msuva aanza kutupia Al-Qadsiah
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
