Manchester, England
Ujumbe wa mawasiliano ya simu kati ya staa wa zamani wa Man Utd, Ryan Giggs na aliyekuwa mpenzi wake, Kate Greville umesomwa mahakamani jana katika kesi inayomkabili Giggs. Katika moja ya ujumbe huo, Giggs anamwambia Kate kwamba anampenda kuliko mechi zote alizocheza za Ligi Kuu England (Giggs amecheza mechi zaidi ya 600 za ligi hiyo kuanzia 1992 hadi 2014) na kisha mahakama ikasomewa mashairi ya Giggs kwa Kate.
Ujumbe huo uliokuwa ukisomwa mbele ya mahakama ulihusisha mawasiliano ya wawili hao kuanzia Oktoba 2013 hadi 2018 ulizingatia matukio yalivyokuwa yakijitokeza hatua kwa hatua kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Giggs mwenye umri wa miaka 48 anatuhumiwa kwa kumpiga Kate na mdogo wake Emma tukio lililotokea Novemba Mosi 2020 nyumbani kwa Giggs jijini Manchester pamoja na tuhuma nyingine za ubabe na udhalilishaji dhidi ya Kate, matukio ambayo anadaiwa kuyafanya kati ya mwaka 2017 na Novemba 2020 ingawa tayari amekana tuhuma hizo.
Ilielezwa mahakamani hapo kwamba Giggs na Kate walikuwa na tabia ya kutumiana ujumbe huo kwa muda mrefu wakati wa mahusiano yao ambayo yanadaiwa kuanza mwishoni mwa mwaka 2013 ambapo kwa wakati wote huo wamekuwa wakigombana na kupatana hadi usiku wa tukio la Kate kupigwa akiwa na mdogo wake, Emma ambaye anadaiwa kutishwa.
Mawasiliano ya ujumbe wa Giggs na Kate yaliyosomwa mahakamani jana yalikuwa kama ifuatavyo…
Giggs: “Wewe ni wa kipekee, ni msichana anayenifurahisha kuliko wasichana wote niliowahi kukutana nao.
Kate: Asante, umenishtua
Giggs: Za asubuhi bebi, leo ‘nitakupa upendo’ kama vile siku ya kesho haipo na kesho nitafanya tena hivyo hivyo.
Giggs: Tafadhali bebi usiniache kwenye mataa, sijui kama tuko kwenye mapenzi au hatuko, nakupenda sana bebi, uzuri wako ni wa kipekee.
Giggs: Hakika sijawahi kukufanya unikimbie, naamini ni hivyo Kate?
Kate: Hujawahi, hakika wewe ni wangu haswa, rafiki wangu wa ukweli, huwezi kunifanya nikukimbie, hujawahi hata kujaribu.
Giggs: Kate wewe ni wa aina yake, ni mwanamke anayenivutia zaidi kati ya niliowahi kukutana nao, na navutiwa mno na wewe.
Giggs: Nakupenda kuliko mechi zote nilizoshiriki za Ligi Kuu England, mechi ambazo ni nyingi mno
Giggs: Za asubuhi, huwa najiuliza mwenyewe swali hili, nimewezaje kukuvuta kwangu, wewe ni pambo, mrembo haswaa, ni ndoto yangu ya kipekee.
Giggs: Kate nakupenda hadi kwenye sayari nyingine pamoja na mechi zote nilizocheza za Ligi Kuu England ambazo ni nyingi, nakupenda bebi.
Kate, Giggs bebi, wewe ni dunia yangu, uwe na siku njema mpenzi…
Giggs: Uko poa?
Katika ujumbe mwingine Giggs anamuandikia Kate ujumbe ufuatao ambao ulikuwa katika mtiririko wa mashairi: “Navutiwa na wewe, navurugwa na hisia za mapenzi kwako, nakukubali wewe, siwezi kuishi bila wewe, siwezi kuacha kukufikiria wewe tunapokuwa mbalimbali, wewe ni mwangaza wangu, ni kipenzi cha moyo wangu, ni nguvu yangu, wangu wa pekee, mwenye thamani kwangu, ni mimi na wewe.”
Kate akajibu shairi hilo la Giggs, “Kila siku unanifanya nijivunie wewe kwa sababu unanipa thamani.”
Giggs: “Mpenzi wangu Kate, bila shaka yoyote penzi letu limefika, nilikupenda siku ya kwanza nilipokuona, nakumbuka kwa sababu nilikuwa juu kama kishada, hayo macho mazuri yalinifanya nizizime, sikudanganyi, nakufikiria wewe, nakuota wewe, nikifikiria nilivyokupata naona kama vile nimefanya mapinduzi makubwa yasiyo mfano.
Giggs, “Hilo tumbo, hiyo miinuko mwilini, hizo picha ulizonitumia, umenifanya niwe mwenye furaha, hasa unapokuwa katika mshangao na naanza kufikiri wakati wote uko sahihi, ni sawa, hiyo inatufanya tushikamane, namalizia kwa kusema wewe ni kipenzi changu, rafiki yangu, moyo wangu, na zaidi ya yote unaniamini mimi jambo linalonifanya niwe imara kama mti.
Kimataifa Giggs alimtumia Kate mashairi ya mapenzi
Giggs alimtumia Kate mashairi ya mapenzi
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
