Na mwandishi wetu
Mtibwa Sugar imeamua kuzima fununu za kuinasa saini ya kipa Mkenya, Faroukh Shikalo baada ya kumtambulisha rasmi sambamba na straika Mrundi, Matore Pipi.
Taarifa za kutua kwa Shikalo katika timu hiyo ambayo leo inaumana na Singida Big Stars kwenye mechi ya kirafiki, zilianza kuelezwa mapema baada ya kipa huyo kuiaga KMC mwishoni mwa msimu uliopita.
Mbali na utambulisho wa Shikalo na Pipi, pia Mtibwa imetangaza kumnasa, Eliuter Mpepo aliyekuwa Mbeya City ambaye pia amewahi kuzitumikia GD Interclub ya Angola na Cape Umoya ya Afrika Kusini.
“Huu ni usajili mkubwa kwetu, hawa vijana wanafahamu kazi yao ndiyo maana tumewachukua kuja kuongeza nguvu kikosini,” alisema Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru.
“Mfano huyu Pipi ni kijana wa kazi kweli anajua majukumu yake na kama ulivyoona kama misimu miwili hivi tunatetereka, sasa ni muda wa kukaa sawa na kurejesha ukongwe na uthubutu wa kikosi chetu kama kinavyojulikana,” alisema Kifaru.
Soka Shikalo asaini Mtibwa Sugar
Shikalo asaini Mtibwa Sugar
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
