Munich, Ujerumani
Klabu ya Bayern Munich inaendelea kujiimarisha baada ya kuondoka kwa mshambuliaji wao nyota Robert Lewandowski na tayari imemsajili kwa mkataba wa miaka mitano beki wa Uholanzi, Matthijs de Ligt aaliyekuwa akikipiga Juventus ya Italia.
De Ligt ambaye ndio kwanza ana miaka 22, amejiunga na Bayern kwa ada ya Pauni milioni 65.3, alisajiliwa Juventus mara ya kwanza Julai 2019 na kudumu na vigogo hao wa Serie A kwa misimu mitatu na sasa anahamia katika Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga.
Akiwa na Juventus, De Ligt amefanikiwa kutwaa taji la Serie A mara moja na Coppa Italia mara moja na hadi anaondoka ameichezea timu hiyo mara 117 katika mashindano tofauti.
“Nina furaha kuwa mchezaji wa klabu kubwa, Bayern ni moja ya klabu zenye mafanikio Ujerumani, ni moja ya klabu yenye mafanikio Ulaya na duniani. Nina furaha kwani sasa nakuwa sehemu ya historia ya Bayern, ni klabu ye kipekee inayoendeshwa kwa malengo makubwa,” alisema De Ligt.
De Ligt pia alikuwa akiwindwa na Chelsea kabla ya Bayern kuipiga bao na anakuwa mchezaji wa pili kutoka Uholanzi kujiunga na Bayern katika msimu huu wa usajili baada ya kiungo, Ryan Gravenberch.
Bayern pia imeshawasajili mshambuliaji Sadio Mane kutoka Liverpool na beki wa kulia Noussair Mazraoui kutoka Ajax huku ikiwa imeondokewa na mshambuliaji wake mahiri, Lewandowski aliyejiunga na Barcelona kwa ada inayotajwa kufikia Euro milioni 50.
Kimataifa Bayern yamng’oa beki Juventus
Bayern yamng’oa beki Juventus
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
