London, England
Mpango wa mshambuliji Neymar kuondoka katika klabu ya Paris St-Germain (PSG) ya Ufaransa umezidi kuwa mgumu baada ya Man City ambayo ilihusishwa na mipango ya kumchukua mchezaji huyo kudai kuwa haimhitaji.
PSG ilikuwa tayari kumtoa Neymar, 30 kwa makubaliano ya kubadilishana na mchezaji wa Man City, Bernardo Silva lakini Man City ambao ndio vinara wa Ligi Kuu England wanadaiwa kutokuwa tayari kwa mpango huo.
Neymar inaonekana hayafurahii maisha ya PSG na anakumbukwa kuzomewa yeye na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo baada ya kutolewa na Real Madrid katika hatua ya 16 bora kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mbali na Man City, mchezaji huyo pia aliwahi kuhusishwa na mipango ya kujiunga na Chelsea ambapo, Mbrazil mwenzake. Thiago Silva aliwahi kunukuliwa akiufurahia mpango huo kwa kusema kwamba klabu hiyo inamfaa Neymar lakini Chelsea nayo haionekani kuvutiwa na mpango wa kumsajili mchezaji huyo.
Mambo ya baadaye ya Neymar katika klabu ya PSG aliyojiunga nayo mwaka 2017 akitokea Barcelona yanaonekana kuwa si mazuri na ndio maana anatafuta pa kutokea hasa ikizingatiwa kwamba hata bosi wa klabu hiyo Sheikh Nasser Al Khelaif aliwahi kutoa kauli ya kutoridhishwa na mafanikio ya timu hiyo akiwalaumu wachezaji mastaa.
Kimataifa Man City yamkataa Neymar
Man City yamkataa Neymar
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
