London, England
Kiungo wa zamani wa Arsenal na timu ya Taifa ya England, Jack Wilshere ametangaza kustaafu soka akiwa na miaka 30.
Wilshere ambaye pia amewahi kuzichezea klabu za Bolton, West Ham, Bournemouth pia za England na AGF Aarhus ya Denmark, amepata umaarufu zaidi akiwa klabu ya Arsenal ambayo ameichezea mechi 197 na kushinda kombe la FA mara mbili tangu ajiunge na timu hiyo akiwa kijana mdogo wa miaka 16.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwenye mitandao ya kijamii, Wilshere ambaye pia ameichezea timu ya Taifa ya England mara 34 alisema anaona kama mambo yake katika soka yamekuwa ndivyo sivyo katika siku za karibuni.
“Ni safari ya kipekee ambayo imechanganyika na matukio ya kuvutia na naona ufahari kupitia katika yote hayo ambayo nimeyafanya katika maisha yangu ya soka,” alisema Wilshere.
“Kutoka kuwa kijana mdogo anayecheza mpira kwenye bustani hadi kuwa nahodha wa timu niipendayo ya Arsenal na kuichezea nchi yangu kwenye fainali za Kombe la Dunia, hakika nimetimiza ndoto yangu.”
Februari mwaka Wilshere alijiunga na AGF, amecheza mara 36 tu tangu atoke Arsenal mwaka 2018, majanga ya kuwa majeruhi yamekuwa yakimuandama na kukaa bila ya kuwa na timu yoyote katika msimu wa 2020/21.
“Ukweli ni kwamba imekuwa vigumu kukubali kwamba kipaji changu kimeondoka katika siku za karibuni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu licha ya kwamba nimekuwa nikijiona bado nina mengi ya kufanya,” alisema.
Kimataifa Wilshere astaafu akiwa na miaka 30
Wilshere astaafu akiwa na miaka 30
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
