Manchester, England

Beki wa Manchester City, Benjamin Mendy amehusishwa na makosa mengine mawili ya ubakaji na moja ya udhalilishaji kijinsia.
Mendy mwenye umri wa miaka 27 anatarajia kuripoti katika mahakama ya Stockport leo Jumatano na sasa atakuwa akikabiliwa na makosa sita ya ubakaji baada ya manne ya awali sambamba na moja la udhalilishaji kijinsia.
Mashtaka hayo yanatokana na matukio ambayo yanadaiwa kufanywa na mchezaji huyo kati ya Oktoba 2020 na Agosti mwaka huu yakihusisha wanawake wawili tofauti wa umri unaozidi miaka 16 na msichana mmoja wa umri chini ya miaka 18.
Mendy ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa, amekuwa akiiwakilisha vyema Man City tangu mwaka 2017 alipojiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Monaco ya Ufaransa.
Msimu ulioipita Mendy alishiriki vyema katika mafanikio ya timu hiyo hadi kutwaa taji la Ligi Kuu England lakini tangu ahusishwe na tuhuma hizo klabu yake imemsimamisha ikisubiri upelelezi wa polisi ukamilike.
