Na mwandishi wetu
Injinia Hersi Said ataendelea kuiongoza klabu ya Yanga kwa kipindi kingine cha miaka minne baada ya kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumapili, Agosti 2, 2026.
Ushindi huo umekuja katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa klabu hiyo ambapo kiongozi huyo hakuwa na mpinzani kama ilivyokuwa kwa makamu wake, Arafat Haji ambao wataendelea kuiongoza klabu hiyo.
Katika nafasi za wajumbe watano wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo, walioshinda ni Munir Seleman, Alexander Ngai, Yanga Makaga, Julius Koi na Fahd Afif.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Hersi aliwataka wanachama wa klabu hiyo kuvunja kambi zilizotokana na makundi ya uchaguzi na kuwa kitu kimoja.
Kwa upande wa wagombea walioshindwa katika uchaguzi huo, Hersi aliwataka kutoyapokea matokeo hayo kwa chuki kwa kuwa wao bado ni wanachama wa Yanga.
Hersi aliwapongeza wagombea ambao wamefanikiwa kushinda katika nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji wakiwamo wawili aliosema kuwa ni wapya na wengine watatu wamebaki.
“Wagombea waliokosa nafasi nao ni washindi licha ya kwamba kura hazikutosha, hawatakiwi kuwa maadui wa klabu yetu badala yake wanapaswa kuwa sehemu ya klabu yao,” alisema Hersi.
Katika mkutano huo, Hersi pia alipata nafasi ya kuwaeleza wanachama mafanikio ya uongozi wake tangu akabidhiwe jukumu hilo takriban miaka minne iliyopita.
Kimataifa Hersi apewa miaka mingine minne Yanga
Hersi apewa miaka mingine minne Yanga
Read also
