Barcelona, Hispania
Rais wa klabu ya Barcelona ya Hispania, Joan Laporta ametangaza kujiuzulu wadhifa huo ingawa anatarajia kuingia katika mbio za kuwania kiti hicho katika uchaguzi utakaofanyika Machi 15 mwaka huu.
Kanuni za klabu hiyo zinamtaka rais wa klabu aliye madarakani kujiuzulu wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi na kamati ya uongozi itapewa jukumu la kusimamia shughuli za kila siku za klabu kwa kipindi hicho.
Kamati hiyo itakuwa chini ya Rafa Yuste ambaye amekuwa mmoja wa makamu wa Laporta tangu achaguliwe katika nafasi hiyo mwaka 2021.
Katika uchaguzi wa nafasi hiyo, Laporta anatarajia kuchuana na Xavier Vilajoana, Joan CamprubÃ, VÃctor Font na Marc Ciria ambao wote kwa nyakati tofauti wametangaza nia ya kuwania kiti hicho.
Taratibu za uchaguzi katika klabu hiyo zinamtaka kila anayetaka kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi awe na saini za wajumbe wa klabu hiyo 2,321 ili jina lake liwemo katika orodha ya wagombea.
Laporta alichaguliwa kwa mara ya pili mwaka 2021 akiwa rais wa Barcelona au Barca baada ya kushikilia wadhifa huo kati ya mwaka 2003 na 2010, aliibuka mshindi katika chaguzi za mwaka 2003 na 2006.
Uchaguzi wa safari hii wa klabu hiyo kampeni zake zinatarajia kutawaliwa na mambo kadhaa ikiwamo usajili wa wachezaji katika majira ya kiangazi, masuala ya fedha, maendeleo ya ujenzi wa uwanja na nafasi ya nyota wao wa zamani Lionel Messi katika klabu hiyo kwa siku zijazo.
Kimataifa Rais wa Barcelona ajiuzulu
Rais wa Barcelona ajiuzulu
Read also
