Tunis, Tunisia
Baada ya kukumbana na matokeo ya aibu kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026, Tunisia imemteua kocha Mfaransa Herve Renard kuchukua nafasi ya Sabri Sabri Lamouchi aliyebwaga manyanga.
Shrikisho la Soka Tunisia limethibitisha juu ya uamuzi huo Jumatatu Juni 16, 2026 na kubainisha kuwa Renard atabeba majukumu ya timu hiyo maarufu The Eagles ikiwa ni mkakati wa kusaka matokeo mazuri.
Tunisia imezianza vibaya fainali hizo kwa kupokea kichapo cha mabao 5-1 mbele ya Sweden katika mechi yao ya kwanza, matokeo ambayo yameiweka timu hiyo mkiani katika Kundi F.
Mtihani wa kwanza wa Renard utakuwa Jumamosi, Juni 20 katika mechi yao ya pili dhidi ya Japan, mechi ambayo inaweza kufufua matumaini ya timu hiyo kutoishia hatua ya makundi.
Renard ni mmoja wa makocha wanaoheshimika katika soka hasa barani Afrika na moja ya mafanikio yao ni pale alipoiwezesha timu ya taifa ya Zambia ‘Chipolopolo kubeba taji la Afcon 2012.
Miaka mitatu baadaye akiwa na timu ya Ivory Coast, Renard kwa mara nyingine aliiwezesha timu hiyo kubeba taji la Afcon.
Renard pia amewahi kuwa kocha Morocco na Saudi Arabia, akiwa na timu ya Saudi Atabia kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 zilizofanyika Qatar, timu yake iliushtua ulimwengu kwa kuifunga Argentina, timu ambayo baadaye ndiyo iliyoibuka bingwa wa dunia.
Kimataifa Renard Herve abebeshwa zigo Tunisia
Renard Herve abebeshwa zigo Tunisia
Read also
